Psalms 9

Shukrani Kwa Mungu Kwa Ajili Ya Haki Yake

(Kwa Mwimbishaji: Mtindo Wa Muth-Labeni.
Muth-Labeni ni mtajo mmojawapo katika lugha za muziki.
Zaburi Ya Daudi)


1
Zaburi hii ikiunganishwa na ya 10 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
cEe Bwana, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.

2 dNitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.


3 Adui zangu wamerudi nyuma,
wamejikwaa na kuangamia mbele zako.

4 eKwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu;
umeketi kwenye kiti chako cha enzi,
ukihukumu kwa haki.

5 fUmekemea mataifa na kuwaangamiza waovu;
umeyafuta majina yao milele na milele.

6 gUharibifu usiokoma umempata adui,
umeing’oa miji yao;
hata kumbukumbu lao limetoweka.


7 h Bwana anatawala milele,
ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu.

8 i jMungu atahukumu ulimwengu kwa haki,
atatawala mataifa kwa haki.

9 Bwana ni kimbilio la watu wanaoonewa,
ni ngome imara wakati wa shida.

10 kWote wanaolijua jina lako watakutumaini wewe,
kwa maana wewe Bwana,
hujawaacha kamwe wakutafutao.


11 lMwimbieni Bwana sifa, amefanywa mtawala Sayuni,
tangazeni miongoni mwa mataifa, yale aliyoyatenda.

12 mKwa maana yeye alipizaye kisasi cha damu hukumbuka,
hapuuzi kilio cha wanaoonewa.


13 nEe Bwana, tazama jinsi walivyo wengi adui zangu wanaonitesa!
Nihurumie, uniinue kutoka malango ya mauti,

14 oili niweze kutangaza sifa zako
katika malango ya Binti Sayuni
na huko niushangilie wokovu wako.

15 pMataifa wameanguka kwenye shimo walilolichimba,
miguu yao imenaswa kwenye wavu waliouficha.

16 q Bwana anajulikana kwa haki yake,
waovu wamenaswa katika kazi za mikono yao.


17 rWaovu wataishia kuzimu,
naam, mataifa yote wanaomsahau Mungu.

18 sLakini mhitaji hatasahaulika siku zote,
wala matumaini ya walioonewa hayatapotea.


19 tEe Bwana, inuka, usimwache binadamu ashinde.
Mataifa na yahukumiwe mbele zako.

20 uEe Bwana, wapige kwa hofu,
mataifa na yajue kuwa wao ni watu tu.
Copyright information for SwhKC